Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga alamba dili la Ubalozi

Mandonga Balozi Karim Mandonga akitangazwa kuwa balozi wa duka la Mr Discount Dar es Salaam.

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Hassan Mandonga ametangazwa kuwa balozi wa duka la Mr Discount jijini Dar es Salaam kwa mkataba endelevu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mkurugenzi wa duka la Mr Discount Khalid Mbarak alisema wameamua kumtangaza bondia huyo kutokana na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi pamoja na nidhamu aliyokuwa nayo.

"Nidhamu ndio kila kitu tumeamua kumpa ubalozi mandonga kutokana na kuridhishwa na nidhamu pamoja na utendaji wake wa kazi,alisema.

Alisema mbali na Mandonga vile vile watawapa ubalozi wachezaji wengine wakiwemo wa riadha,mpira wa miguu,Wakati huo huo karim Mandonga aliwataka mabondia pamoja wachezaji wote nchini kuwa na nidhamu kwani nidhamu imemfanya afike mbali kwenye mchezo wa ngumi na kuahidi kufanya kazi yake hiyo kwa nguvu moja.

Alisema amefurahi kupata ubalozi huo na kusema atapambana kuhakikisha anafika mbali kupitia ubalozi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live