Naibu Waziri wa Maji Nishati na Madini, Shaaban Ali Othman amesema kuanza kwa mchezo wa Ngumi ni moja ya kichocheo kikubwa katika kutoa fursa za ajira pamoja na kuimarisha uchumi wa nchi.
Shaaban ambaye aliwahi kuwa Bondia katika mchezo wa ngumi ameeleza hayo wakati wa kutangazwa kwa kuchezwa kwa pambano la kwanza la ngumi tangu kupigwa marufuku kwa mchezo huo na aliyekua Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati, Abeid Amani Karume katika mwaka wa 1964.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko kutoka kampuni ya TOSH, Amitin Abubakar amesema pambano hilo ambalo litachezwa kwa mara ya kwanza Agosti 27, mwaka huu katika uwanja wa Mau na kushirikisha mabondia asilimia 80 kutoka Zanzibar na asilimia 20 kutoka Tanzania Bara.
Miongoni mwa mabondia ambao watatikisa na kutunishana misuli katika pambano hilo ni pamoja na Karim Mandonga, Dula Mbabe, Mussa Nassor Banja pamoja na mabondia mbalimbali wa Zanzibar na Tanzania Bara.