Kuelekea Usiku wa Masumbwi Visiwani Zanzibar Agost 27 mwaka huu, Mabondia Karim Mandonga, Dulla Mbabe na Mabondia wengine zaidi ya 14 wamewasili Visiwani Zanzibar kwa ajili ya ziara maalumu na kupima uzito kulekea mapambano yao ya masumbwi katika Uwanja wa Mao Tsung Mjini Unguja.
Ziara ya Mabondia hao ilianza katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui ambapo walipata fursa ya kusoma Dua katika Kaburi la Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume.
Akizungumza wakati wa Mapokezi ya Mabondia hao Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Idrissa Kitwana Mustafa amesema kuwa, amefarijika kwa kutembelewa na Mabondia hao na kuhakikishia Ulinzi na Usalama kuelekea siku ya Mapambano hayo.
Tazama Video hapa Chini;