Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandoga aja na ngumi mpya akijiandaa kuzichapa na Maarifa

Mandonga Ngumi Mpya Mandoga aja na ngumi mpya akijiandaa kuzichapa na Maarifa

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia Karim Mandonga ametangaza ngumi yake mpya aliyoiita 'Ngumi Sato, ngumi Sangara' atakayotumia katika pambano lisilo la mkanda dhidi ya mpinzani wake, Salum Maarifa kutoka jijini Mwanza.

Mandonga ametambulisha ngumi hiyo leo Ijumaa Septemba 29, 2023 jijini Mwanza wakati wa shughuli ya upimaji wa uzito kuelekea pambano la mkanda kati ya bondia Mtanzania, Fadhir Magiha dhidi ya Mfilipino, Renz Rosia litalopigwa kesho usiku kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza.

"Mabondia wanaokutana na Madonga wanapigwa kama ngoma sasa leo nimekuja na 'Ngumi Sato, ngumi Sangara' njooni Rock City Mall hapo. Hataki anapigwa anataka atapigwa," amesema Mandonga akijinadi kuelekea pambano hilo ambalo halijatambulika ni la raundi ngapi.

Mpinzani wake, Salum Maarifa amesema Mandonga ameyakanyaga wala asitarjie mteremko katika pambano hilo, huku akiwataka mashabiki wasuburie kushuhudia pambano la akili nyingi.

Baadhi ya mabondia waliopima uzito kwa ajili ya kupigana kwenye utangulizi kabla ya pambano la Magiha dhidi ya Mfilipino, Renz Rosia, ni pamoja na bondia machachari, Francis Miyeyusho dhidi ya Said Nkola, Peter Mtera dhidi ya Johnson John na Agness Kayange dhidi ya Stumai Mushi.

Kwa upande wake, Bondia, Stumai Mushi amechimba mkwara mzito na kudai uzoefu wa ndondi aliyoupata katika mapambano yake aliyopigana nchini Uturuki atautumia kumchakaza mpinzani wake, Agness Kayange.

Hata hivyo, Agness amesema hatishiki na maneno ya mpinzani wake badala yake mashabiki wajitokeze kushuhudia Stumai akipasuliwa uso na kumaliza pambano hilo kwa 'TKO'.

Ndondi hizo zilizopewa jina la 'Royal Tour Boxing Kanda ya Ziwa' zinalenga kuhamasisha shughuli za Utalii katika hifadhi za Taifa ikiwemo hifadhi ya Burigi-Chato mkoani Kagera.

Chanzo: Mwanaspoti