Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majiha atetea taji WBC Afrika, Zugo akipigwa KO

Majihaaaaaa Majiha atetea taji WBC Afrika, Zugo akipigwa KO

Sun, 21 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia namba moja nchini na bingwa wa WBC Afrika,Fadhili Majiha amefanikiwa kutetea mkanda wake wa ubingwa wa WBC Afrika kwa kumchapa kwa pointi Sabelo Ngebiyana wa Afrika Kusini huku Abeid Zugo akichapwa kwa KO na Mkenya, Albert Kimario.

Katika pambano hilo la Ngumi imenyooka limefanyika juzi jijini hapa kwenye Ukumbi wa New City Pub, Majiha ameshindakwa ushindi majaji watatu katika pambano hilo la raundi kumi.

Majiha alianza kwa kasi pambano hilo kabla ya kumwangusha chini Sabelo katika raundi ya kwanza aliyewahi kuinuka na kuendelea na raundi zote zilimalizika bila ya kuwepo kwa KO.

Majiha ameshinda pambano hio kwa ushindi wa majaji wote watatu katika pambano hilo ambalo limechezeshwa na Maybin Kante wa Malawi huku jaji wa namba moja wa Tanzania, John Chagu akitoa pointi 99-90 wakati Elton Ndosine wa Malawi huku Erick Khoza wa Afrika Kusini akitoa 98-93.

Mara baada pambano hilo, Majiha alisema kuwa ameshindwa kuonyesha mchezo mzuri licha ya ushindi aliuopata kutokana hali ya hewa wa Mbeya huku akimuomba Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ampelekee zawadi ya mkanda huo kwa kuwa ameshinda akiwa kwenye jimbo lake.

Katika upande mwengine, Abeid Zugo amepoteza pambano kwa KO ya raundi ya nne dhidi ya Albert Kimario ambapo baada ya pambano hilo, Zugo aliwaomba radhi Watanzania huku akidai kuwa amecheza pambano hilo akiwa na majeruhi ya mkono.

Lakini kwa upande wa Idd Pialali amefanikiwa kumchapa kwa pointi Kiaku Ngoy wa DR Congo katika pambano la raundi nane wakati Emmanuel Mwakyembe akimpopoa kwa pointi Gabriel Ochieng wa Kenya.

Mubaraka Denso yeye amefanikiwa kumchapa kwa pointi, George Kandulo wa Malawi huku Kelvin Ngedere akimchapa kwa pointi Yohana Kayuni wakati Mkaveli Mponji akimpiga kwa pointi Erick Muchunguzi huku Emmanuel Amosi akimchapa kwa pointi Nasibu Habibu.

Chanzo: Mwanaspoti