Mabondia 18 wanatarajia kusindikiza pambano kubwa la ngumi litakalomhusisha bondia maarufu nchini Seleman Kidunda dhidi ya bondia raia wa Democrasia ya Congo Patrick Mukala.
Aidha kutokana na uwepo wa mabondia hao vijana, mashabiki wa mchezo wa ngumi wwmeombwa kutazama vipaji vya mabondia wachanga mtaani ili wapewe nafasi ya kuonekana ili kubadilisha mchezo wa Masumbwi na kuwa na Mabondia wengi wenye mafanikio na majina nje na ndani ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam Promota wa Mapambano ya ngumi za kulipwa nchini kutoka KampuniyaKemmon sports Agency, Saada Kasonso amesema wadau na wapenzi wa ndondi wategemee kuona vipaji vipya vya mabondia kutoka Mtaani hususani mabondia wachanga.
“Katika pambano linalokuja ambapo pambano kubwa ni Selemani Kidunda dhidi ya Patrick Mukala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uzito wa kilo 76 wakigombania mkanda ABU raundi 10 litasindikizwa na vijana wapya ambao wana uwezo mkubwa japo walikosa nafasi ya kuonekana kupitia kampuni yetu ya Kemmon Sports Agency, tutawatambulisha vipaji hivyo kwa watanzania".
Saada amewataja mabondia 18 ni Oscar Richard dhidi ya Adam Mbega, Emmanuel Mwakyembe atapigana na Francis Miyeyusho, Mbaraka Mtange atazichapa na Hamza Mchanjo, Alex Kachelewa dhidi ya Adam Mrisho, Mwinyi Mzengela kumenyana na Ajemi Amani.
Wengine Abdul Kubila dhidi ya Msabaha Salum, Omary Baraka kupigana na Muksini Kizota, Ahmady Pelembela dhidi ya Iddy Pazzy wakati Frola Machela atacheza na Halima Bandola.
Akizungumzia pambano hilo, Bondia Selemani Kidunda amesema kutokana na maandalizi mazuri anayofanya, watanzania wategemee ushindi kutoka kwake.
“Nimejipanga na naendelea na mazoezi, bondia ninayeenda kucheza naye ni mzuri, lakini atapigwa na mkanda utabaki nyumbani."
Kidunda mwenye umri wa miaka 39, anapanda ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kushinda pambano ya Kidemkrasi ya Congo (DRC), pambano hilo lilofanyika Julai mwaka jana, Songea mkoani