Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MWAKINYO APANIA KUIREJESHA NDONDI ZANZIBAR

Capture 491?fit=431%2C339 MWAKINYO APANIA KUIREJESHA NDONDI ZANZIBAR

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Bondia nchini Tanzania Hassan Mwakinyo amewasili Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuiomba serikali ya Zanzibar ili iweze kuuruhusu mchezo wa Ngumi hapa Zanzibar.

“Zanzibar kuna vipaji vingi sana hapa lakini hawapati nafasi ya kuonyesha vipaji vyao , kama Zanzibar wataruhusu mchezo huu basi Zanzibar itatowa Mbondia Wakubwa na wakimataifa” amesema Mwakinyo

Mwakinyo ameongeza kuwa amefurahi sana kufika Zanzibar, na Zanzibar ni moja ya sehemu ambayo anayoipenda sana. amesema Mwakinyo

Mratibu wa Hassan Mwakinyo ambae ni Ahmada Salum Suleiman amesema kuwa “Lengo la kuja Mwakinyo kuja Zanzibar ni kuukuza utalii wa ndani na kuutangaza kimataifa ili wageni wavijue vivutio vya Zanzibar wajue kama Zanzibar hakuna Corona napia Mwakinyo amekuja kuweza kufafanua na kuiomba Serikali ya Zanzibar kurejesha mchezo wa Ngumi”amesema Mratibu

Mwakinyo atakuepo Zanzibar kwa takriban Siku mbili atatembelea Vituo vya Habari mbali vya Zanzibar kwa Siku hii ya Leo na kutembelea Vivutio vya Utalii vya Mjini, Usiku atakuepo maeneo ya Forodhani.

Na katika ratiba ya Siku ya Kesho ataonana na Waziri wa Michezo kesho asubuhi na atakuwa na mazungumzo mafupi ya kuonana na Mkuu wa Mkowa wa Kusini Unguja Mh. Ayubu Mohammed Mahmoud na baadae ataelekea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima.

Chanzo: zanzibar24.co.tz