Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya kupigwa, Francis Ngannou kukomba Tsh bilioni 25

Skysports Tyson Fury Francis Licha ya kupigwa, Francis Ngannou kukomba Tsh bilioni 25

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Francis Ngannou, Raia wa Cameroon atalipwa Kiasi Cha Dollar Milioni 10 ambazo ni takribani shilingi bilioni 25 za Kitanzania Katika pambano lake la usiku wa kuamkia jana Dhidi ya Tyson Fury wa Uingereza.

Ngannou atalipwa Fedha hizo zote bila kujali matokeo kama aidha amedundwa au ameshinda, na kwa Upande wa Tyson Fury atalipwa Dollar Milioni 50 sawa sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 150.

Francis Ngannou ambaye ni mshiriki wa mchezo wa Kick Boxing amekuwa akipatiwa mafunzo ya Ubondia na Bingwa wa Zamani wa Ngumi Katika Uzito wa juu Duniani Mike Iron Tyson.

Katika pambano hilo Bingwa wa dunia wa uzito wa juu wa [WBC] Tyson Fury alimshinda bondia huyo wa zamani wa [UFC] Francis Ngannou kwa pointi baada ya uamuzi wa Majaji wawili kwa mmoja katika pambano lisilo la ubingwa lililochezwa nchini Saudi Arabia, pambano ambalo watu wengi waliamini Ngannou alistahili ushindi.

Ngannou alimwangusha Tyson katika raundi ya tatu kwa [left hook] ingawa haikuamua mwenendo wa pambano kwa aslimia kubwa lakini ni kama pambano lote lilitawaliwa na Ngannou kwa ambao tumeangalia pambano hilo hata ukiuliza zaidi ya mara tatu bado Ngannou alistahili kushinda .

Jaji wa kwanza alitoa [95-94] kwa Ngannou, Majaji wengine walitoa [96-93] na [95-94] kwa Fury.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live