Msanii maarufu wa komedi nchini, Musa Kitale amesema kuwa anahisi kuna mkakati kabambe umeandaliwa kwa ajili ya kumshusha bondia namba moja Tanzania, Hassan Mwakinyo.
Kauli hiyo ya Kitale inakuja baada ya Bondia Hassan Mwakinyo kugomea hatapanda Ulingoni kupigana dhidi ya Bondia Julius Indonga kwenye pambano la kuwania mkanda wa IBA International kutogana na Uwongo na kile alichokiita kuwa ni Udanganyifu wa Ma Promota.
"Nilichogundua kwa sasa kutoka kwa watu wa Mchezo wa ndondi asilimia kubwa wanataka kumshusha Mwakinyo kutokana na misimamo yake. Ukisikiliza voice not aliyoweka yule mzee hakuna kosa la Mwakinyo zaidi ya msimamo na kulinda biashara yake zidi ya maadui zake.
"Ni sawa na Marekani kumtumia Ukraine kwa kutaka kumdhoofisha Urusi, alafu Urusi amwambie ndugu yake Ukraine achana na Marekani hao ni maadui zetu wa muda mrefu, Ukraine asione kosa la Marekani kwakuwa yeye hana tatizo na Marekani.
"Kilichokuja kutokea Urusi na Ukraine, wanapigana wenyewe kwa wenyewe huku Marekani katulia, na ndicho kinachoendelea sasa hivi kati ya Mwakinyo na muandaaji wa pambano la Mwakinyo, yule mdhamini katulia zake kwakuwa lengo lake linaenda kutimia," ameandika Musa Kitale.