Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa Mfilipino, Mwakinyo apiga kambi milimani

81703 Pic+mwakinyo Kisa Mfilipino, Mwakinyo apiga kambi milimani

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

UZOEFU wa bondia Arnel Tinampay ni kama umemtisha Hassan Mwakinyo kuelekea pambano lao la Novemba 29 na kulazimika kuhamisha kambi yake iliyokuwa ikifanyika Makorola, Tanga. Mwakinyo sasa ameamua kupiga kambi akijifua katika milima ya Usambara wilayani Lushoto ili kujiweka fiti zaidi kuelekea kwenye pambano hilo. "Nahitaji kutengeneza ufiti wa miguu, nilipokwenda Uingereza ilinigharimu kwa kiasi fulani japo nilishinda (alimchapa Sam Eggington aliyekuwa bondia namba nane wa dunia kwenye uzani wa super welter) lakini mazoezi ya kukimbia katika mashine kule hayakunisaidia, nilipata shida kidogo hivyo sitaki changamoto ile ijirudie" alisema Mwakinyo. Bondia huyo atazichapa pambano la raundi 10 litakalopigwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ambalo kwa mujibu wa waandaaji, wako kwenye mazungumzo na uongozi wa WBF na IBF ili liwe la ubingwa. "Najua ugumu wa pambano linalokuja, umuhimu wa mimi kushinda na kitu gani mashabiki wangu wanahitaji, hivyo sitowaangusha," alisema Mwakinyo ambaye ni balozi wa SportPesa Mpinzani wa Mwakinyo anatarajiwa kuwasili nchini wiki mbili kabla ya pambano ambapo kwa mujibu wa ratiba yake atafanya mazoezi ya wazi eneo la Mlimani City na Mbagara Dar es Salaam na uwanja wa Tangamano Tanga kabla ya kurudi Dar es Salaam tayari kwa pambano.

Chanzo: mwananchi.co.tz