Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana aliyepigwa na Tyson kwenye ndege apata wakili

Tyson Ngumii Kijana aliyepigwa na Tyson kwenye ndege apata wakili

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Abiria wa ndege ya JetBlue aliyepigwa ngumi na bondia maarufu duniani Mike Tyson (55) amepata wakili wa kumuwakilisha katika kesi yake inayotajwa kuwa ya madai ya fidia kutoka kwa bondia huyo.

Wakili wa Abiria huyo amesema mteja wake ni shabiki mkubwa wa Mike Tyson, jivyo alipagawa na kupata furaha ya kupitiliza baada ya kumuona nguli huyo wa masumbwi wa muda wote wakati wakiwa pamoja kwenye ndege hiyo.

Wiki hii video ilisamba ya Tyson akigombana na abiria kwenye ndege ambapo baadae mashahidi walisema 'Alikuwa shabiki aliyepitiliza kuwa na furaha [Overly Excited Fan] alikuwa na shauku kubwa na kumuona Tyson akajisahau na kumsumbua zaidi."

Wakili wa kijana huyo anasema kwa bondia mkubwa kama Tyson anayejua vizuri sheria za ngumi hakupaswa kuchukua maamuzi ya kumpiga shabiki wake badala yake angewaita wahudumu wa ndege na wangejua cha kufanya kumdhibiti shabiki huyo badala ya kujichukulia hatua za kumtwanga ngumi nzito mpaka kumpasua uso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live