Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo ngumi atangaza neema kwa mabondia

51693 NGUMI+PIC

Thu, 11 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Joe Anea amesema moja ya mikakati yake ni kurejesha heshima ya mchezo huo nchini kwa kuwaibua akina Rashid Matumla wapya.

Anea alisema katika uongozi wake atafanya kazi na kila mdau wa ngumi bila kujali tofauti zilizojitokeza kwenye mchakato wa uchaguzi uliofanyika Machi 31, Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), Anea alisema changamoto zilizokuwepo kwenye mchezo huo zinaelekea ukingoni.

“Kulikuwa na ubabaishaji mwingi, mabondia walipewa mikataba feki na ushahidi tunao, wengine walishinikizwa kuuza mapambano, vurugu zilikuwa nyingi kwenye ngumi,” lakini sasa ngumi zitakaa katika mstari.

Alisema wameanza kurejesha heshima ya mchezo huo ili Tanzania irudi katika ubora wa kimataifa, wadhamini warudi na mabondia wanufaike na jasho lao.

“Tumeanza kuweka misingi mizuri tumekuwa na mawasiliano na vyama vya ngumi vya kimataifa, mtandao wa ngumi wa dunia (Boxrec) ambavyo vyote vimeridhia kufanya kazi na sisi japo awali ilikuwa ngumu kutokana na taarifa ambazo walikuwa wamelishwa na watu ambao hawakutaka kuona TPBRC inafanikiwa,” alisema Anea.

Alisema ngumi za kulipwa zimewekewa utaratibu wa uhakika ambapo wamekomesha suala la mikataba feki lililokuwa likifanywa na mawakala hapa nchini.

“Sasa bondia anapopata pambano nje ya nchi, Kamisheni imekuwa ikiwasiliana moja kwa moja na promota wa nje ili kupata mkataba halali, zamani pambano la Dola 8000, bondia alitengenezewa mkataba feki wa dola 3000, ambazo nazo aligawana na wakala, lakini sasa tumekomesha hilo,” alisema Anea.



Chanzo: mwananchi.co.tz