Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigogo atajwa, Mwakinyo akitetea taji kimyakimya

Mwakinyo Alivyopata Ushindi Kigogo atajwa, Mwakinyo akitetea taji kimyakimya

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Saa 24 tangu kukwama kuzichapa Ijumaa na kujiweka hatarini kupoteza mkanda wa WBO Afrika kwa uzito Middle, hatimaye bondia Hassan Mwakinyo alilazimika kucheza juzi Jumamosi kimyakimya dhidi ya Patrick Allotey kutoka Ghana na kushinda kwa TKO raundi ya tatu na kutetea taji hilo.

Awali, pambano hilo lilikwama kupigwa Ijumaa kwenye Ukumbi wa Warehouse, Masaki baada ya Msimamizi wa mkanda huo, Samir Captain kugoma kuibuka ukumbini kwa kilichoelezwa hajalipwa fedha na promota wa pambano hilo, lakini zikafanyika juhudi juzi nchana kutwa na mwishowe usiku wake likapigwa.

Katika pambano hilo, lililochezwa bila kurushwa hewani na Azam TV na kuhudhuriwa na mashabiki wachache bila kiingilio, Mwakinyo alipata ushindi huo baada ya Allotey kushindwa kurudi ulingoni kwa ajili ya raundi ya tatu kwa madai ameumia bega na hivyo refa wa mchezo kumaliza pambano lililokuwa la raundi 10.

Kwa matokeo hayo, Mwakinyo ametetea taji hilo alililotwaa Januari 28, mwaka huu kwa kumpiga kwa KO ya raundi ya saba, bondia kutoka Ghana, Elvish Ahorgah.

Awali, kabla ya Mwakinyo kulazimika kuzichapa na Allotey, msimamizi wa pambano hilo, Samir alitoa masharti ya kulipwa fedha zake kabla ya saa 12 jioni ya juzi, la sivyo angesepa zake na taji na hivyo bondia huyo Mtanzania angepoteza mkanda, kitu kinachoelezwa kiliingiliwa kati na kigogo mmoja wa serikali.

“Kigogo huyo aliamua kuingilia kati, ili kuhakikisha pambano linapigwa usiku huo huo, ili kuona Mwanyiko hapotezi mkanda na kwa bahati mpinzani wake alichomoa kuendelea kabla ya kuanza kwa raundi ya tatu kwa kutorudi ulingoni na refa kutoa ushindi kwa Mtanzania,” kilisema chanzo kutoka kwenye kikao kilichowezesha pambano hilo kuchezwa kilichomhusisha pia Mwakilishi wa WBO nchini, Emmanuel Mlundwa aliyedokeza mapema kuwa Mwakinyo na Allotey wangezichapa usiku huo.

Chanzo: Mwanaspoti