Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kidunda, Tony Rashid ulingoni Februari 24

Kidunda Vs Tony Rashid Kidunda, Tony Rashid ulingoni Februari 24

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabondia wawili nguli wa Tanzania, Seleman Kidunda na Tony Rashid, watapanda ulingoni Februari 24, katika pambano la kimataifa litakalofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es salaam.

Kidunda atapambana na Patrick Mukala wa DR Congo mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, wakiwania ubingwa wa ABU uzito wa Super Middle.

Wakati Tony atapambana kuutetea ubingwa wake wa ABU uzito wa Super Bantam, dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini.

Mbali na mapambano hayo mawili, kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi siku hiyo.

Promota wa pambano Hilo Saada Salum kutoka KEMMON SPORTS AGENCY amesema mabondia wote tayari wamesaini na maandalizi ya pambano yanaenda vizuri kufikia sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live