Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kidunda: Mabondia tupimwe dawa za kuongeza nguvu

Kidundaaa 1 At 11.jpeg Kidunda: Mabondia tupimwe dawa za kuongeza nguvu

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Selemani Kidunda ametaka mabondia wanaokuja kupigana nchini wapimwe matumizi ya dawa za kuongeza nguvu sababu kuna baadhi wanahusishwa kutumia dawa hizo zisizoruhusiwa michezoni.

Kidunda amesema utaratibu uliopo kwa sasa mabondia wakipigana nchini hawapimwi matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni kama wafanyavyo nchi nyingine, badala yake hapa nchini wanapima uzito na afya tu.

“Nilivyopigana juzi na bondia kutoka Afrika Kusini kuna watu walinifuata kwenye kona yangu wakaniambia mwenzako kuna vitu anakula wakihisi labda ni dawa za kuongeza nguvu, sasa baada ya mechi alitakiwa apimwe lakini hapa halifanyiki hilo," amesema Kidunda.

Amesema utaratibu wa kupima mabondia dawa za kuongeza nguvu dakika kadhaa kabla ya pambano na baada ya pambano, itaongeza chachu ya mabondia kufanya mazoezi zaidi na atapatikana bigwa halali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live