Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kidunda Bingwa mpya Mkanda wa WBF Intercontinental

Kidunda Seleman Sele.jpeg Seleman Kidunda amemchapa kwa pointi Tshimanga Eric Katompa

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Mtanzania Seleman Kidunda ameibuka mshindi katika Pambano la masumbwi dhidi ya Mkongo Tshimanga Eric Katompa na kutawazwa kuwa Bingwa mpya wa mkanda wa WBF Intercontinental.

Seleman kidunda na Eric Katompa walikuwa wakigombea ubingwa wa WBF Intercontinental SuperMiddle Weight.

Pambano la leo lilikuwa ni la marudiano baada ya Pambano la awali kumalizika kwa sare baada ya Kidunda kupata majeraha katika raundi ya tatu mechi ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam Disemba 2021.

Pambano hili lilikuwa ni la Raundi kumi 10 na limepigwa katika Uwanja wa Maji Maji Songea, Mkoani Ruvuma.

Dalili za ushindi kwa Seleman Kidunda zilianza kuonekana mwishoni mwa raundi ya pili baada ya kufanikiwa kumsukumia konde zito mpinzani wake, na kuonekana kumuelemea hivyo Kidunda kutawala sehemu kubwa ya mchezo.

Katompa alizinduka raundi za mwishoni lakini tayari Kidunda alishajikusanyia alama za kutosha kutoka kwa wajaji wa mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live