Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiduku akata tamaa kwa Mwakinyo

3df516631520bae0b45cb90709fb515d Kiduku akata tamaa kwa Mwakinyo

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BONDIA wa ngumi za kulipwa, Twaha Kiduku amesema baada ya Hassan Mwakinyo kukataa kupambana naye hawezi kumlazimisha tena na sasa anasubiri wengine wa kiwango kama chake.

Mwaka uliopita nyota huyo alionesha dhamira ya kutaka kupambana na Mwakinyo ambae mashabiki wake wanamuita Tanzania One lakini bondia huyo mwenyeji wa Tanga alimjibu kuwa si wa viwango vyake.

Akizungumza na HabariLEO Dar es Salaam jana, Kiduku alisema hataki kumlazimisha mtu tena na anaheshimu maamuzi yake, hivyo anaendelea kujifua kuimarisha kiwango chake kwa ajili ya mapambano mengine yatakayotokea mbele.

“Kwa sasa naendelea kujifua na kujiweka tayari kwa pambano lolote lijalo, Mwakinyo nilishakata tamaa kwake siwezi kumlazimisha,” alisema bondia huyo anayeishi Morogoro.

Kiduku alisema kutokana na ubora wake, pambano lolote litakalokuja hatokubali kiurahisi bila kuangalia maslahi.

“Liwe pambano la nje au ndani ni lazima niangalie maslahi nitanufaika vipi sio kushiriki ilimradi kama ambavyo wengine wanafanya,” alisema.

Kiduku ni miongoni mwa mabondia hatari nchini kutokana na ubora alioonesha mwaka uliopita, akifanya vizuri katika mapambano aliyocheza nyumbani.

Ubora wake ulivuma zaidi baada ya kumpiga mpinzani wake mkubwa, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ mwaka jana hali iliyomfanya kujiamini na kutamani kukutana na Mwakinyo akiamini na uwezo wa kumwangusha. Kiduku amecheza mapambano 22 na kati ya hayo ameshinda 16, amepoteza sita na kutoka sare moja.

Chanzo: habarileo.co.tz