Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiduku, Lamthuam ulingoni leo

A3107255aa4fb217e9901136f6eb3061.jpeg Kiduku, Lamthuam ulingoni leo

Fri, 30 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BONDIA, Twaha Kassim ‘Kiduku’ leo anatarajiwa kuzichapa na Mthailand Sirimongkhon Lamthuam kutoka Thailand katika pambano la kimataifa la kuwania mkanda wa WBC litakalochezwa katika Uwanja wa PTA, Sabasaba.

Ni pambano muhimu hasa kwa Kiduku ambaye ni mchanga katika ndondi kujitahidi ili kutengeneza rekodi bora itakayopandisha viwango vyake.

Kiduku alipata fursa hiyo kubwa baada ya kuonesha uimara katika pambano dhidi ya Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’.

Mpinzani huyo wa Kiduku ni mzoefu aliyecheza mapambano 101 na kati ya hayo ameshinda 97 na kupoteza manne.

Hiyo ni rekodi kubwa ambayo pengine Kiduku anakutana na mtu aliyemzidi katika ubora hivyo atakapompiga atakuwa katika viwango vya juu.

Kwa upande wa Kiduku, amecheza mapambano 22 na kati ya hayo ameshinda 15, amepoteza sita na kupata sare moja.

Akizungumzia maandalizi yake, bondia huyo alisema amejipanga vizuri na yuko tayari kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuhakikisha anashinda pambano hilo.

“Nitakikisha nawakilisha vizuri mkoa wangu wa Morogoro na Taifa, nimefanya maandalizi ya kutosha naamini nitashinda,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz