Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kichapo cha Wilder chashtua mabondia

Foighters Kichapo cha Wilder chashtua mabondia

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipigo cha bondia Deontay Wilder kutoka kwa Joseph Parker kimewashtua wengi kwenye masumbwi ya uzito wa juu. Parker amemchapa Wilder kwa pointi katika pambano lililofanyika Riyadh, Saudi Arabia.

Pambano hilo lilitajwa ni muhimu kwa ajili ya kuandaliwa kwa pambano lake na Anthony Joshua, ambaye pia alimchapa Otto Wallin kwa TKO kwenye raundi ya tano.

Kitendo cha Wilder kushindwa linafanya pambano lake la AJ sasa kuwekwa kiporo. Lakini, matokeo hayo ya pambano la Wilder ma Parker yana maana gani kwa mabondia wengine wa uzito wa juu kama Tyson Fury, Oleksandr Usyk na Daniel Dubois? Cheki hapa nini kitatokea kwa kila bondia wa uzito wa juu.

-Deontay Wilder; Bondia Wilder alipaswa kupambana na Joshua kwenye pambano lake lijalo kama angefaniwa kumchapa Parker. Mshindi kwenye pambano hilo basi angekuwa na shughuli ya kupigana na ama Tyson Fury au Oleksandr Usyk. Lakini, kushindwa kwa Wilder kunaweka kwenye mashaka makubwa juu ya pambano lake la Joshua, licha ya makubaliano ya kusaini mkataba wa Pauni 100 milioni.

Sasa Wilder atalazimika kutafuta njia nyingine ya kutafuta pambano lake la Joshua litokee. Na hapo anaweza kupigana tena na Parker ili kuweka uhai wa pambano lake na Joshua.

-Anthony Joshua; Bondia Joshua pambano lake na Wilder litachukua muda kabla ya kufanyika. Bondia huyo aliweka mazingira mazuri ya pambano hilo kutokea baada ya kumchapa Otto Wallin huko Saudi Arabia. Promota wa Joshua, Eddie Hearn aliwahi kusema pambano dhidi ya Filip Hrgovic ndilo litakalofuata. Lakini, mipango yake ni kupambana pia na mshindi baina ya pambano la Tyson Fury na Oleskandr Usyk, ambao kama wataweka kipengele cha kurudiana kwenye mkataba wake, watamfanya Joshua asubiri zaidi.

-Tyson Fury; Akili ya Tyson Fury kwa sasa ipo kwenye pambano lake lijalo dhidi ya Oleksandr Usyk. Mabondia hao watazipiga Februari 17 mwakani huko Saudi Arabia. Na mshindi kwenye pambano hilo atapigana na Joshua kama hakutakuwa na kipengele cha kurudiana. Fury anahitaji sana kuzipiga na Joshua, lakini hilo litatokea kufuatia matokeo yake atakapozipiga na Usyk.

-Oleksandr Usyk; Kama ilivyosemwa, mechi ya marudiano kati yake na Tyson Fury inaweza kupangwa baada ya pambano lao la kwanza. Usyk hajapoteza, lakini Fury ana ubora mkubwa wa kumpatia kichapo cha kwanza bondia huyo wa Ukraine. Pambano la mabondia hao linasumbuliwa kwa hamu, huku Daniel Dubois na Joshua wote wakiwataka mabondi hao.

-Daniel Dubois; Bondia Dubois atakuwa na shughuli ya kupigana na Fury au Usyk kwenye pambano lake lijalo. Dubois anahitaji pia kuzipiga na Joshua, lakini Mwingereza mwenzake huyo kuna uwezekano akataka kupigana kuwania mkanda wa IBF kwenye pambano lake lijalo.

Jambo hilo linamfanya Dubois kuwa na pambano la kuzipiga na ama Fury au Usyk, kama mabondia hao wawili wasiopigika hawatarudiana. Na kama hilo litokea, basi Dubois atasubiri wakati wake ufike na huenda akaanza kwa kupigana tena na Joe Joyce au kuzitajwa na Parker kwenye pambano lijalo.

Chanzo: Mwanaspoti