Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaseba aibuka kidedea TPBA,Dulla Mbabe mjumbe

Japhet Kaseba[1] (1) Mwenyekiti wa kwanza wa TPBA, Japhet Kaseba

Sun, 8 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Bingwa wa ngumi na mateke (Kick Boxing) Tanzania, Japhet Kaseba, ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha mabondia wa ngumi za kulipwa Tanzania (TPBA) kwenye uchaguzi wa chama hicho uliofanyika mapema leo.

Kaseba anakuwa mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, akipata kura za ndio 26 na kumshinda mpinzani wake Mada Maugo aliyepata kura za ndio 16.

Nafasi ya Katibu Mkuu imeenda kwa Salum Mgeni aliyepata kura 36, wajumbe wawili ni Francis Miyeyusho aliyepata kura 24 na Fatuma Yazidu aliyepata kura 25.

Naye Bondia Dullah Mbabe akiangukia katika nafasi ya ujumbe kwa kupata kura 20.

Chanzo: eatv.tv