Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Karim Mandonga achezea tena kichapo, asisitiza ajali kazini

Karim Mandonga TKO.jpeg Bondia Karim Mandonga

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia mwenye maneno mengi kutoka Mkoani Morogoro Karim Mandonga kwa mara nyingine amechezea kichapo katika pambano la "Usiku wa Visasi" dhidi ya Shabani Kaoneka pambano lililopigwa katika Uwanja wa Majimaji Songea.

Mandonga anaesifika kwa majigambo na tambo alipigwa kwa TKO katika raundi ya nne ya pambano la utangulizi dhidi ya Shabani Kaoneka.

Akizungumza baada ya Pambano mandonga amesema;

"Hii ni kama ajali kazini, mtu anayependa kazi na asiyependa ajali inamkuta, lakini simuhofii Shaban Kaoneka, naweza sema pia ni mipango ya mungu amepanga nipoteze na mimi sina uwezo wa kumbishia mungu"

Mandonga amekuwa maarufu nchini licha ya kupoteza mapambano yake mawili yaliyopita kutokana na tambo zake anazozionesha kabla ya mapambano yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live