Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kambi ya Mfaume Mfaume yatamba

Mfaume Mfaume Kambi ya Mfaume Mfaume yatamba

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Bondia Mfaume Mfaume, Ramadhan Uadi ‘Rama Jah’ ametamba bondia wake kumpiga mpinzani wake Nkululeko Mhlongo wa Afrika Kusini na mashabiki waamue ampige raundi ya ngapi.

Rama Jah ametoa kauli hiyo ya tambo ikiwa ni wiki chache kabla ya pambano hilo lililopewa jina la ‘Hata usipolala Patakucha tu’ litakalofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam Juni 30.

Amesema wamejiandaa vizuri na wanaendelea na maandalizi kuelekea kwenye pambano hilo ambapo licha ya kutomdharau mpinzani huyo, bado ana uhakika bondia wake ataibuka na ushindi.

“Binafsi niwaachie mashabiki waamue Mfaume Mfaume ashinde kwenye raundi ya ngapi, tunamuheshimu mpinzani wetu kutokana na rekodi zake lakini bado kwenye mzani Mfaume Mfaume atashinda sina wasiwasi na hilo,” amesema Rama Jah na kuongeza,

“Mpinzani tunamheshimu kwa rekodi yake na ubora wake, ana nyota mbili na nusu ni zaidi ya bondia wangu lakini nina uhakika wa ushindi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live