Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaka bondia punguza kasi basi

Mwakinyo Aahidi Kumchapa Kuvesa Katembo Bondia Hassan Mwakinyo

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Braza wetu bondia kutoka Pwani ya Kaskazini ujue watu wanakukubali sana ila kuna nyakati unaamua kwa makusudi kuwafanya wakuponde.

Sawa, tunafahamu kuwa kuongea sana ndio utamu wa mchezo wa ngumi lakini basi yale unayoyaongea yahusu ngumi na sio kuingia kazi za watu ambazo wewe hazikuhusu.

Waponde na wanange mabondia wenzako hadi uchoke tutakusapoti kaka lakini ukiingia katika upande ambao wewe huna utaalam nao basi hapo jiandae kukosolewa na kiufupi wewe ni mwanadamu unakosea kama wanavyokosea wengine.

Juzi juzi tu kaka umesikika na kuonekana ukisema kuwa unataka kukiomba kituo cha luninga ambacho kimekuwa kikionyesha mapambano mengi ya ngumi kwamba pindi unapokuwa ulingoni na pambano, wachambuzi wa pambano lako wasiwe mabondia wenzako.

Inavyooneka braza unaamini mabondia wenzako hawachambui vizuri mapambano yako na hivyo basi kazi hiyo wawe mabondia wastaafu au wachambuzi wa kawaida ambao sio mabondia kwa maana kwamba hao ndio unadhani watachambua kwa haki.

Hapo kaka haukuwa sahihi kwa sababu hilo wewe sio jukumu lako ukizingatia kwamba unakuwa umeshalipwa stahiki zako na kinachobakia kwa upande wako ni kupanda ulingoni upigane na bondia ambaye imepangwa ukutane naye.

Bondia mwenzako akichambua pambano lako, wewe unakuwa hauathiriki chochote kwa vile hana nafasi ya kukufundisha wewe au kumsaidia bondia unayepigana naye hivyo haupaswi kuwa na hofu katika hilo.

Chombo cha habari kinakuwa kimelipia fedha ya haki za matangazo ambazo kati ya hizo kuna nyingine zinakuja kwako kaka hivyo kiache kiamue chenyewe ni kipi kinafaa kwa maslahi yake na wateja wake ili kiweze angalau kurudisha kile ambacho imekitoa ili kufanikisha wewe upigane.

Tupo katika nyakati za kuzingatia weledi braza hivyo kila mmoja anatakiwa atekeleze wajibu na majukumu yake pasipo kuingilia ya mwingine.

Kama wewe ulilazimisha bondia fulani asipigane katika utangulizi wa pambano lako basi jaribu kuvumilia chombo cha habari kijipangie wachambuzi wake ilimradi hakivunji sheria na utaratibu.

Chanzo: Mwanaspoti