Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua amchapa Ruiz arudisha mataji yake IBF, WBA na WBO

87604 Pic+joshua Joshua amchapa Ruiz arudisha mataji yake IBF, WBA na WBO

Thu, 12 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Riyadh, Saudi Arabia. Bondia Anthony Joshua amefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa dunia wa ngumi uzani wa juu baada ya kumchapa kwa pointi Andy Ruiz Jr katika pambano la marudiano lililofanyika Saudi Arabia.

Miezi sita baada ya usiku ambao Ruiz aliushangaza ulimwengu wa ngumi, Joshua amelipa kisasi kwa kufanikiwa kunyakuwa ubingwa wa IBF, WBA na WBO.

Baada ya kufanikiwa kumpasua sehemu ya juu ya jicho Ruiz katika raundi ya kwanza, Joshua alitumia ngumi zake nyingi kulenga katika eneo hilo akitumia konde lake la mkono wa kulia pamoja na jabs jambo lililofanya mashabiki 14,000kuanza kuimba "AJ, AJ, AJ" kwenye ukumbi wa Diriyah Arena.

Ruiz hakuonekana kama angefanikiwa kupata KO hata pambano lilipokwisha majaji walitoa pointi 118-110 118-110 na 119-109, jambo lililomfanya Joshua kurukaruka kwa furaha ulingoni hapo akishangilia ushindi wake dhidi ya mtu aliyempiga Juni nchini Marekani.

Joshua (30), sasa anaungana na kundi la mabondia wachache waliofanikiwa kurudisha mikanda yao baada ya kuipoteza wakiwemo Muhammad Ali, Lennox Lewis, Evander Holyfield, Mike Tyson na Floyd Patterson.

Akizungumza baada ya pambano hilo Joshua amekubali kupigana kwa mara ya tatu na Andy Ruiz Jr iwapo atakuwa tayari.

“Kama upo tayari basi kutapambana kwa mara nyingine” alisema Joshua.

Ruiz aliongeza: “Sitaki kutoa kisingizio. Kama tutapata nafasi ya kupigana kwa mara ya tatu litakuwa ni jambo jema kwa maisha yangu.

“Nafiriki nitakuja nikiwa bora zaidi, naamini pambano lijalo nitajianda vizuri zaidi na timu yangu,” alisema Ruiz.

Promota Eddie Hearn hakutaka kusema lolote kuhusu uwezekano wa pambano la marudiano.

Alisema: Mtazamo wa baadaye ni kusherekea na kusherekea, Joshua ameshinda ubingwa wa Olimpiki na usiku huu Saudi amekuwa bingwa wa dunia wa uzito wa juu kwa mara ya pili.

“Usiku huu ameshinda kwa uamuzi wa majaji, tumpe heshima yake kwa hilo.”

Chanzo: mwananchi.co.tz