Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua ajilipua kwa Fury

Fury Vs Joshua Decemberr Fury, Joshua kuvaana Disemba

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye ulimwengu upo karibu kabisa kushuhudia pambano kubwa la ngumi baina ya waingereza wawili kwenye uzito wa juu duniani (heavyweight), Anthony Joshua dhidi ya Tyson Fury, watakaopigana mwezi Desemba 3 mwaka huu.

Pambano hilo limethibitishwa leo, kufuatia bondia Anthony Joshua 'AJ' kukubali ofa aliyokuwa amepewa na Tyson Fury kufuatia bondia aliyetakiwa kupigana naye kutoka Ukraine, Oleksandr Usyk 'kuchomoa' kwa madai ya kujiuguza majeraha na akataka pambano lao lipigwe mapema mwakani.

Hata hivyo, tayari Fury alishaamua kutaka apigane mwaka huu ili kukata kiu ya mashabiki wake kumuona ulingoni, kitendo cha Usyk kukwepa kupigana ndani ya mwaka huu ndicho kilichomfanya amchague AJ awe tayari kupigana naye kabla ya kujiandaa na pambano la Usyk mwakani.

Katika sehemu ya ofa hiyo aliyotoa Fury kwa AJ, ni kuweka mkanda wake wa WBC alionao ambao aliutetea kwa Deontay Wilder na akaamua kustaafu masumbwi kabla ya kutengua ili apigane na Usyk aliyemchapa Joshua mara mbili mtawalia. Sehemu ya ofa hiyo ni kupata asilimia 40 kati ya 100 za donge la pambano hilo.

Matchroom, kampuni inayomsimamia Joshua ndio imethibitisha kukubali ofa hiyo leo na wapo tayari kupigana na Fury Desemba 03 baada ya awali kutaka pambano liwe Desemba 17 ambayo ilikataliwa na upande wa Fury chini ya promota wake Frank Warren.

Warren amethibitisha wazi kuwa, mkataba wa pambano hilo utawafikia upande wa Joshua wakati wowote na tangazo la mpambano huo utawekwa sawa ikiwemo mgongano uliopo kwa pande za mabondia hao kwenye kampuni walizoingia nazo mkataba wa kuonyesha mapambano yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live