Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua: Ruiz akinipiga tutarudiana kwa mara ya tatu

87166 Pic+joshua Joshua: Ruiz akinipiga tutarudiana kwa mara ya tatu

Thu, 5 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Diriyah, Saudi Arabia. Bondia Anthony Joshua amemuhaidi Andy Ruiz Jnr yuko tayari kurudiana kwa mara ya tatu kama atafanikiwa kutetea ubingwa wake katika pambano lao la Jumamosi usiku.

Pambano hilo la tatu sasa linaonekana litakuwepo baada ya Joshua kuzungumzia uwezekano wake katika mazoezi yake ya jana usiku.

Joshua alisema: 'Inawezekana tukaonana kwa mara ya tatu endapo Andy ataendelea kuwa bingwa. Nipo tayari kupigana naye. '

Kushuka kwa joto kulimfanya Joshua kushindwa kuvua t-shirt na kuonyesha mwili wake uliopungua.

Hata hivyo Joshua alizungumzia kuhusu uzito wake: 'Sijabadilika kitu chochote. Malengo yangu ni kushinda.Kutakuwa na pambano la kukata na shoka Jumamosi, lakini jambo la muhimu ni kushinda.'

Ruiz ambaye alimshinda Joshua mwezi Juni 1 na kushinda mataji ya WBA, IBF, WBO na IBO katika usiku moja, pia alisema kuhusu kupungua kwake uzito kwa lengo la kuongeza wepesi na kasi yake.

Ruiz alisema: 'Mtaona mambo mengi mazuri kutoka kwangu katika pambano la Saudi Arabia. '

Chanzo: mwananchi.co.tz