Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua: Nimeshinda sawa, ila sina furaha

Anthony Joshua D Anthony Joshua

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa uzito wa juu, Anthony Joshua amefichua licha ya kushinda pambano lake dhidi ya mpinzani wake, Jermaine Franklin lakini hana furaha kutokana na aina ya uwezo ambao aliweza kuuonyesha katika pambano hilo.

Bondia huyo juzi Jumamosi alipanda ulingoni dhidi ya Franklin na kufanikiwa kushinda kwa pointi za majaji wote kwa matokeo ya 118-111, 117-111 na 117-111.

Mara baada ya ushindi huo bondia huyo, 33, aliliambia Sportsmail kuwa hana furaha kwa namna ambavyo aliweza kucheza pambano hilo lakini anashukuru kwa kuwa alishinda.

“Sina furaha kwa namna nilivyocheza leo (juzi) kwa kuwa nilikuwa natakiwa kuonyesha uwezo wa juu zaidi lakini nashukuru nimeweza kushinda.

“Kwa sasa najua kile ambacho mashabiki wanakita¬ka. Wam¬emtaja Tyson Fury, mpira upo kwenye mikono yake.

"Litakuwa jambo la heshima kupambana na bingwa wa uzito wa juu wa WBC duniani. Kama ananisikia, anamjua promota wangu, tulikuwa na mazungumzo kabla, sasa tunatakiwa kuendelea na hilo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live