Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jesca: Ubondia usiwachanganye, kwenye mapenzi sijiwezi

Jesca Mfinanga Bondia wa kike Jesca Mfinanga

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia wa kike Jesca Mfinanga (22) wa uzani wa kilo 60, amesema anapokuwa ulingoni anavaa sura ya kazi ni tofauti na akiwa nyumbani na mpenzi wake ambapo upole na adabu vinatawala.

Mfinanga ambaye hivi karibuni amepoteza pambano la Boxing on Boxing day dhidi ya Sara Alex wa Arusha aliyemshinda kwa pointi, amesema laiti watu wangejua upande wake wa pili kuhusu mapenzi angewashangaza.

"Si unaniona nilivyo mrembo, kwa mpenzi wangu sina sauti, najitambua ndio maana naweza nikatofautisha kazi na nafasi yangu kwa mtu wangu,"amesema na kuongeza;

"Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa mwenyeji wa Tanga, alinishangaza kuniambia tuachane ana mwili wa mapenzi hivyo hataki mwanamke bondia, maana tulikuwa na malengo ya kuoana,maneno ya watu ndio yalimtisha, ila wa sasa anapenda kazi ninayofanya na ananisisitiza nifanye mazoezi."

Amesema kupitia kazi hiyo, anawafundisha watu wanaotaka kupunguza mwili na vitambi amekuwa akijipatia ridhiki ya kuendesha maisha yake.

"Kingine watu wasichojua, nimesomea uandishi wa habari ingawa sikumaliza hadi mwisho baada ya ada kukata, nikaamua kuingia kwenye ngumi kutumia nguvu zangu mwenye kujipatia kipato, ndio maana huwezi kunikuta natembea kwa kudundika, kazi za nyumbani nafanya zote,"amesema.

Jesca aliingia rasmi kwenye ngumi 2019 kwa kupewa sapoti na nguli wa mchezo huo, Japhet Kaseba anayemuita baba yake mlezi"Namwita baba kwani amefanya nijulikane, amekuwa akiunga mkono juhudi za vijana wengi wanaopenda kufika mbali kwenye mchezo huo."

Chanzo: Mwanaspoti