Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Msangi, promota wa ngumi asiyeishiwa mikasa

Msangi+pic Jay Msangi, promota wa ngumi asiyeishiwa mikasa

Wed, 30 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By IMANI MAKONGORO Mwenyewe anasema jina tapeli sio geni kwake. Ndilo linamtambulisha haraka kwenye ramani ya ngumi nchini, lakini anasisitiza kuwa ndiye promota anayefanya mapambano ya ngumi za kulipwa yenye mvuto nchini.

Jay Msangi, promota wa ndondi asiyeishiwa mikasa ya mara kwa mara katika mapambano anayoandaa.

Tangu aingie kwenye ndondi kwa mara ya kwanza na kuandaa pambano kubwa la ubingwa wa dunia wa WBF kati ya Francis Cheka na Phil Williams wa Marekani, Msangi amekuwa na msururu wa mikasa. “Nimekuwa ‘black listed’ lakini kwa nia mbaya, wengi wamekuwa wakinituhumu kwa vitu ambavyo sivyo,” anasema promota huyo.

Msangi anasema maono na uwezo mkubwa katika kuandaa mapambano ndiyo unamfanya kuingia kwenye matukio ya mikasa ya mara kwa mara.

Alipoingia kwenye ramani ya ndondi alifanya ‘promo’ kubwa katika mchezo huo ikiwamo kumleta bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Frans Botha nchini kushuhudia pambano la Cheka na Phil Williams, lakini baada ya pambano hilo aliishia kufungiwa. “Watu walijua nimeingia kutapeli, lile lilikuwa pambano langu la kwanza kufanya nchini, ugeni wa nchi ukasabababisha baadhi ya watu kunizunguka.”

Katika pambano hilo lililopigwa 2013 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, mabondia wa Tanzania akiwamo Cheka waligoma kupanda ulingoni hadi walipwe fedha.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz