Bingwa wa zamani wa dunia kwenye mchezo wa Kick boxing, Japhet kaseba amesema kubwa bondia Abdallah pazi maarafu kama Dulla Mbabe, bado ana 8nafasi ya kufanya vizuri licha ya kupoteza mapambana mawili mfulilizo.
Siku ya Oktoba 8, 2021 Dullah Mbabe, aliwasononesha Watanzania baada ya kuchapwa kwa pointi na Tshimanga Katompa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika pambano la raundi 10 liliofanyika katika ukumbi wa PTA, Temeke Jijini Dar es Salaam.
Kaseba ambaye amewahi kumfundisha Pazi, kwa nyakati tofauti katika ngumi za ridhaa amesema kuwa Pazi anahitaji kuungwa mkono katika kipindi hiki kigumu, hii ikiwa na kuambatana na viongozi ambao watamsaidia kisaikolojia na kumrudisha katika utimamu wa mwili na akili.
Akiwa pia amewahi kushinda ubingwa wa Taifa wa PST pamoja na TPBC, Kaseba ameihasa Jamii kuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono mabondia wa nyumbani pindi wapombana na mabondia kutoka nje ya Tanzania.
“Ukienda Wembley, London uwezi ukakuta waingereza wakimshangilia bondia kutoka nchi nyingine, wanapenda vitu vyao, hivyo ndivyo Watanzania wanakamkuta wanapaswa kufanya pindi mabondia wetu wanapeperusha bendera ya nchi iwe ndani au nje ya nchini’’ Amesema Kaseba.
Dullah ambaye Agosti 20 mwaka huu alishindwa pia kwa pointi na Mtanzania mwenzake, Twaha Kassim ‘Kiduku’, ametangaza kupumzikakwa kwa muda wa miezi miwili na ameahidi kurejea Disemvba 29, 2021 kwenye pambano la Usiku wa Mabingwa.