Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jake Paul : Nitapigana na Alvarez na Logan sio Fury

Jake Vs Woodley 768x542.png Jake Paul vs Woodley

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Jake Paul ameweka wazi kwamba anaweza kupigana na bondia Saul ‘Canelo’ Alvarez pia ndugu yake Logan Paul lakini amefunga milango kwa bondia Tommy Fury.

Staa huyo wa mtandao wa YouTube ambaye ameingia kwenye fani ya masumbwi atarejea uwanjani Jumamosi usiku katika mechi ya marudiano dhidi ya Tyro Woodley baada ya kuchukua nafasi ya Fury ambaye hayupo sawa kiafya.

“Nitapigana na Canelo 100%. Muangalie Avni Yildirim [ambaye Canelo alimpiga mapema mwaka huu]. Jinalake la utani ni ‘The Turkish Warrior’.

“Alikaa chini kwenye kona na kuacha. Hakurusha ngumi hata moja.

“Mimi ni mkubwa zaidi yake. Nina nguvu.

“Sio kuhusu ni muda gani umefanya kitu. Ni kuhusu umefanya vizuri kwa kiasi gani.”

“Siwezi kupigana na Tommy haiwezi kutokea, nahitaji kumuona akipigana mara 20 zaidi.’ aliongeza Jake Paul

Chanzo: www.tanzaniaweb.live