Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ishu ya Mwakinyo kutopigana ipo hivi

Mwakinyo Hajapigana Ishu ya Mwakinyo kutopigana ipo hivi

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameshindwa kupanda ulingoni kutetea mkanda wa WBO Afrika kutokana aliyekuwa promota wa pambano hilo, Shomari Kimbau kumzingua mwakilishi wa WBO, Samir Captain kutoka Ghana.

Mwakinyo usiku wa kuamikia leo alitakiwa kupanda ulingoni kutetea ubingwa huo dhidi ya Patrick Allotey wa Ghana, lakini hata hivyo, haikuwezakana baada ya mwakilishi wa WBO kugomea kufika ukumbini na maofisa waliotakiwa kuchezesha pambano hilo baada ya kucheleweshewa malipo, jambo ambalo lililikwamisha ambalo awali lilitangazwa kuzuiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC).

Mapema jana mchana, Mwanaspoti lilimtafuta na kumuuliza kama kila kitu kipo sawa kuelekea pambano hilo la ubingwa, ambapo alijibu kwa kifupi kuwa hayapo sawa kwa kuwa bado kuna pesa hawalipwa japokuwa hakutaja kiasi, huku akiweka angalizo uwezakano wa kushindikana kwa pambano.

Lakini usiku kwenye Ukumbi wa Warehouse uliopo Masaki, mwakilishi huyo ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu alishindwa kutokea licha ya kupigiwa simu na badala yake aliamua kujifungia hotelini muda wote kabla ya viongozi wa juu wa TPBRC kumpelekea 'difenda' la polisi katika hoteli aliyofikia, lakini haikuweza kusaidia kumtoa kiongozi huyo.

Kutokana na hali hiyo, Mwakinyo na mpinzani wake walilazimika kupanda ulingoni saa 8:15 usiku na kuzungumza na mashabiki juu ya changamoto hiyo, licha ya kila mmoja kudai kuwa yupo tayari kupigana, lakini wamekwamishwa na tatizo hilo.

"Mashabiki wangu, niwaombe radhi kuna jambo limetokea lipo nje ya uwezo wetu japo viongozi wanapambana kulimaliza kwa sababu anayetakiwa kusimamia pambano hajafika hapa," alisema Mwakinyo na kuongeza:

"Niwaombe tuendelee kuvuta subira. Nawaomba sana mashabiki wangu msiondoke kwa kuwa mmekuja hapa kwa ajili yangu na nina kiu ya kuonyesha nilicho nacho."

Lakini kwa upande wa mpinzani wake, alisema: "Hapa Mwakinyo wala mimi hakuna mwenye makosa kwa sababu tupo tayari (kupigana), lakini kuna mambo ya ovyo ya viongozi ndiyo tatizo, hivyo sitegemei kupigana usiku huu kwa sababu mpaka sasa hakuna kinachoendelea."

Baada ya kutoa kauli hizo, mabondia hao walishuka na kuendelea kusubiri kabla ya mwakilishi wa WBO nchini, Emmanuel Mlundwa kuingia ukumbini saa 9 usiku na kufanya kikao kidogo wakitaka pambano hilo lifanyike asubuhi ya leo Jumamosi kwa lengo kumsaidia Mwakinyo asivuliwe ubingwa.

Chanzo: Mwanaspoti