Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrahim Class aisubiri Zanzibar kwa hamu

Image 136 1140x640.png Bondia Ibrahim Mgenda ‘Class’

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Bondia Ibrahim Mgenda ‘Class’ ameeleza kuwa kwa sasa yuko kwenye maandalizi makubwa ya kuhakikisha anaibuka na ushindi kwenye pambano lake litakalopigwa Agosti 27, mwaka huu dhidi ya Khamis Muathai kutoka Zanzibar.

Pambano hilo ambalo ni la kwanza tangu kuruhusiwa kwa ngumi visiwani Zanzibar itapigwa kwenye Ukumbi wa Mao Tse Tung Kisiwani Unguja.

Class amesema kuwa anaamini ataondoka na ushindi katika usiku huo kwa sababu anahisi hakuna bondia mwingine anayejipanga kimazoezi kama yeye nchini Tanzania hivyo ushindi kwake ni kitu cha kusubiri siku ya tukio ifike.

Yaani hiyo tarehe 27 sitaki lawama kwa kweli nawaambia Zanzibar nafanya mazoezi ya kila rangi, nafanya mazoezi ya kila aina na nafanya zaidi ya mara 10, sina imani kwa kweli hapa Tanzania kama kuna bondia anafanya mazoezi zaidi yangu na hilo nitawathibitishia tarehe 27, Khamis ajipange, amesema Class.

Mbali na pambano hilo, mapambano mengine yatawakutanisha Abdllah Pazi ‘Dulla Mbabe’ dhidi ya Banja Hamis na Karim Mandonga atakayezichapa na Muller Junior.

Chanzo: Dar24