Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrah Class aomba radhi kwa TPBRC

Ibra Classs Msamaha Ibrah Class aomba radhi kwa TPBRC

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Ibrahimu Class ameomba radhi kwa mashabiki zake, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Azam TV, waandaaji wa pambano, majaji na Watanzania wote kutokana na maneno yake aliyoyataja kuwa ya kadhia ambayo aliyatoa dhidi ya Kamisheni ya Ngumi pamoja na majaji usiku wa Jumamosi kwenye #TheJungleFight jijini Arusha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ibrahimu Class ameweka taarifa inayosema kuwa

"Nimetazama kwa umakini pambano lote la Dullah Mbabe dhidi ya Eric Katompa na naomba msamaha , niliyoyasema ni hisia zangu tu"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live