Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibra Class atamba kumchakaza Pina

Class Pic Data Bondia wa ngumi za kulipwa, Ibrahim 'Class' Mgender

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia wa ngumi za kulipwa, Ibrahim 'Class' Mgender ukipenda mwite 'King Class Mawe' ametamba kusambaratisha mpinzani wake, Gustavo Alan Pina kutoka Mexico katika pambano litakalofanyika Ijumaa Septemba 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar-Es-Salaam

Class amesema amejiandaa vyema kuelekea mpambano huo baada ya kumaliza programu ambayo alikuwa amepewa na kocha wake.

"Kikubwa ninachoomba ni sapoti ya wadau wangu na wazidi kuniombea ili niwe vizuri hadi siku ya pambano na nifanye kile ambacho wengi wanatarajia kukiona.

"Nina kiu kubwa ya kuwapa 'sapraizi' mashabiki wangu ambao walikuwa wakiingoja kwa muda mrefu, najua nakutana na bondia mzuri kuliko wote ambao nimewahi kukutana nao," anasema Class.

Anasema kulingana na umuhimu wa mchezo huo na jinsi alivyomtazama mpinzani wake, atajitahidi kuwapa mashabiki wake raha kutokana na mpinzani wake atakavyoingia ulingoni.

Mapambano ya utangulizi siku hiyo, Lulu Kayage atazichapa na Sandra Mohamed, Mwinyi Mzengela na Sabari J, Abraham Ndauendapo atakipiga na Alfred Lamptey.

Mapambano mengine ya utangulizi, Jose Hernandez dhidi ya Juma Choki, Emmanuel Mwakyembe na Nicolaus Mwangi, Adam Mrisho atazichapa na Samwel Pandya.

Mara ya mwisho Class kupanda ulingoni ilikuwa Julai Mosi mwaka huu alipozichapa dhidi ya Peter Pambeni wa Zimbabwe na kupata ushindi 'TKO' baada ya Mzimbabwe huyo kuumia mkono raundi ya kwanza.

Chanzo: Mwanaspoti