Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury vs Usyk Pambano la Kihistoria usiku wa leo

Fury Vs Usyk Leo Fury vs Usyk Pambano la Kihistoria usiku wa leo

Sat, 18 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabondia wakali wa uzito wa juu duniani, bingwa wa dunia wa WBC muingereza Tyson Fury na bingwa wa dunia wa WBA, IBF, WBO na IBO m-ukraine Oleksandr Usyk, watapambana kwa raundi 12 usiku wa leo kwenye uwanja wa Kingdom Arena mjini Riyadh, Saudi Arabia, kumsaka ‘Undisputed Champion’ wa uzito wa juu.

Awali pigano hilo lilipaswa kufanyika Februari 17 mwaka huu, lakini lililazimika kupangiwa tarehe mpya baada ya Fury kuumia mazoezini. Kwenye mchezo wa masumbwi ‘Undisputed Champion’, ni bondia anayeshikilia mataji makubwa manne ya masumbwi duniani (WBA, WBC, IBF & WBO) kwa wakati mmoja.

Katika historia ya masumbwi duniani, bondia wa mwisho kuwa ‘Undisputed Champion’ kwenye uzito wa juu alikuwa Lennox Lewis, wakati ule ‘Undisputed Championship’ ni mikanda mitatu (WBA, WBC & IBF) baada ya kumchapa Evander Holyfield Novemba mwaka 1999 pale Thomas & Mack Center mjini Las Vegas.

Hadhi ya Lennox kuwa ‘Undisputed Champion’’ ilikoma April mwaka 2000 baada ya kuuachia mkanda wa WBA kwa kukataa kucheza na mpinzani wa lazima ‘Mandatory Challenger’ wa WBA, John Ruiz, na badala yake akaenda kucheza na mpinzani wa lazima wa WBC, Michael Grant na kushinda KO raundi ya pili.

Hivyo, tangu mwaka 2000 hadi kabla ya pambano la usiku wa leo, ni miaka 24 imepita bila ya uzito wa juu kuwa na ‘Undisputed’ Champion’, iwapo kama leo atapatikana mshindi basi atakuwa ‘Undisputed’ Champion’ wa kwanza wa uzito huo baada ya miaka 24 na wa kwanza katika historia ya uzito huo tangu zama za mikanda minne zianze mwaka 2007.

Kwenye makubaliano ya kimkataba, Tyson Fury atapata 70% na Usyk atapata 30% ya mgawanyo wa fedha (Purse Bid Share) hivyo Fury anakadiriwa kuweka kibindoni kiasi cha Dola za Marekani karibu milioni 150, sawa na Shilingi za Tanzania Bilioni 388 na Milioni 500.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live