Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury v Oleksandr: Mabondia ambao hawajawahi kupigwa wanakutana kuzichapa

Fury V Oleksandr: Mabondia Ambao Hawajawahi Kupigwa Wanakutana Kuzichapa Fury v Oleksandr: Mabondia ambao hawajawahi kupigwa wanakutana kuzichapa

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Bondia wa Uingereza Tyson Fury (35), atamenyana na Oleksandr Usyk (36) wa Ukraine mjini Riyadh, Saudi Arabia tarehe 17 Februari.

Fury anajivunia rekodi ya kutopigwa na kushinda mara 34 na sare moja.

Usyk, 36, ndiye bingwa wa WBA, WBO na IBF huku Fury akishikilia mkanda wa WBC.

Pambano hili litafanyika miezi michache tangu Fury kupata ushindi mwembamba dhidi ya Francis Ngannou huko Saudi Arabia mwezi Oktoba.

Usyk naye ameshinda mapambano yake yote 21 na mwezi Agosti alimpiga Daniel Dubois kutoka London.

Chanzo: Bbc