Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury kumkalisha Whyte wembley? Otto naye atamani

FURY VS WHYE Bondia Tyson Fury Kushoto na Dillian Whyte kulia

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Kwa miaka kadhaa ulimwengu wa masumbwi umekuwa ukitamani kuona pambano la taji la uzito wa juu la kumpata bingwa asiyepigwa, na sasa baada ya kusubiri kwa muda hatimaye njia imeonekana wakati bingwa wa uzito wa juu wa WBC Tyson Fury akiwa ndio mtu anayepewa nafasi kubwa ya kufanya hilo.

Fury atapanda ulingoni jumamosi hii April 23 kutetea ubingwa wake wa WBC dhidi ya Dillian Whyte, ambapo wababe hao wa masumbwi ya uzito wa juu duniani watachapana makonde kwenye uwanja wa Wembley kesho Jumamosi ya April 23, huku Whyte akidhamiria kumvua ubingwa wa WBC Tyson Fury, huku Fury nae akitaka kutete mkanda wake.

(Bondia Otto Wallin)

Kueleka pambano hilo Bondia mwingine wa uzito wa juu duniani Otto Wallin amedai yuko tayari kukabiliana na bondia yoyote kati ya Tyson Fury, Dillian Whyte au Anthony Joshua, huku akieleza ni jinsi gani anaweeza kushinda pambano hilo kama litatokea.

Wallin kwasasa yuko London kwa ajili ya kazi na kustarehe, pia kufuatilia pambano la Wyte na Fury, huku akijitahidi kuweka jina lake katika kila mazungumzo linapokuja suala la masumbwi ya uzito wa juu haswa wakihushwa mabondia Fury na Whyte watakaopanda ulingoni jumamosi hii.

(Bondia Tyson Fury Kushoto na Dillian Whyte kulia baada ya kupima uzito) 

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akifanya kazi na kituo cha Television cha Uswidi wakati wa maandalizi ya kutetea taji la Tyson Fury dhidi ya Dillian Whyte na ametumia fursa hiyo kukumbusha ulimwengu nia yake ya kuingia ulingoni kwa wasimamizi wa ligi hiyo.

Wallin, pia alielezea kuwa anampango kupigana na mpinzani ambaye bado hajathibitishwa mwezi Juni mwaka huu.

Chanzo: eatv.tv