Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury alivyoendelea kumtajirisha Usky

Usyk Life Fury alivyoendelea kumtajirisha Usky

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Heshima mjini. Vijana wengi wanapenda kusema baada ya kupata mafanikio hasa pesa. Juzi usiku Mei 18, Aleksandr Usyk alimkalisha Tyson Fury pambano la raundi 12, lakini kwa pointi za majaji na unaambiwa pambano hilo limempa pesa za maana.

Licha ya ubabe wa Fury lakini Usyk alionyesha ni mwamba kutoka Ukraine na kumtingisha Mwingereza huyo kunazidi kumpa heshima mjini na maokoto yanaongezeka.

Pambano hilo lililopigwa Kingdom Arena, Riyadh huko Saudi Arabia kwa matajiri na si bure mbali na pesa aliyopata ya pambano hilo, maokoto yatazidi kumiminika kutokana na mikataba aliyoingia na madili mengine.

Tajiri anayezidi kuwa tajiri, ndio. Usky pia ana miradi mingi inayomwingizia pesa na kumfanya aishi kibosi mjini.

ANAPIGAJE PESA

Ana utajiri unaokadiriwa kufikia Pauni 45 milioni na uliongezeka zaidi baada ya kumpiga Anthony Joshua mwaka 2022 na alipata Pauni 42 milioni kama malipo ya ushindi.

Hilo ndio lilikuwa pambano lake lililompa pesa nyingi na pambano lake la juzi dhidi ya Fury alipata Euro 40 milioni wakati mwenzake alipata Pauni 100 milioni.

Pia alipata Dola 6 milioni kama pesa za ushindi baada ya kumpiga Daniel Dubois kwa KO.

Mbali ya mapambano hayo Usyk pia anapata pesa nyingi kutokana na biashara zake mbalimbali na ni mmiliki mwenza wa kampuni ya ‘Ready to Fight’

Bondia huyu mwenye umri wa miaka 37, pia ni mmiliki wa kampuni ya Usyk-17 Promotions, inayojihusisha na uandaaji wa mapambano mbalimbali ya ngumi pamoja na kusimamia mabondia.

NDINGA

BMW M8 Gran Coupe-Dola 138,800

Mercedes-AMG-Dola 190,000

Smart Fortwo -Dola 24,650

Audi RS Q8 -Dola 125,800

MSAADA KWA JAMII

Anamiliki taasisi yake iitwayo Usyk Foundation ambayo imejikita zaidi kusaidia wananchi wa Ukraine waliothirika na vita inayoendelea nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, taasisi hiyo imetoa msaada wa zaidi ya Dola 1 milioni hadi sasa ikiwa ni pamoja na chakula.

MJENGO

Anamiliki mjengo wa kifahari huko Vorzel, Ukrane ambayo baada ya vita kuanza,jeshi la Urusi liliteka eneo hilo ikiwa pamoja na nyumba yake lakini mwaka 2022 jeshi la Ukraine likafanikiwa kulikomboa na kupitia mtandao wa Instagram , Usky alipiga picha mbalimbali mara yake ya kwanza kurudi katika nyumba hiyo. Haijajulikana hasa thamani ya nyumba hiyo lakini ripoti zinaeleza haizidi Dola 1 milioni.

MAISHA NA BATA

Kwa sasa yupo katika ndoa na Yekaterina, ambaye alimuoa mwaka 2009, hadi sasa wana watoto watatu ambao ni Kyrylo, Yelizaveta Mykhailo Usyk.

Bondia sio mtu wa kupenda kuweka mambo yake mengi wazi na muda mwingi huuwekeza zaidi kwenye kujifua na kujiweka sawa kwa ajili ya mapambano.

Chanzo: Mwanaspoti