Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury akoleza moto pambano lake na Wilder

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Bondia Tyson Fury amedai siku ya leo itakuwa ‘maalumu’ katika pambano lake na Deontay Wilder.

Fury alisema amejiandaa vyema kushinda na ametoa onyo kwa mpinzani wake kusubiri kipigo.

Pambano hilo la uzito wa juu duniani, limepangwa kuchezwa leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Staples Center, Los Angeles nchini Marekani usiku wa kuamkia kesho Jumapili.

Alisema atapanda ulingoni akiwa na furaha na amejiandaa kufurahia mchezo huo akiwa ulingoni.

Bondia huyo mwenye miaka 30, anarejea ulingoni baada ya kuwa nje ya ulingo kwa miezi sita.

Fury alisema anarejea ulingoni akiwa mpya baada ya kupunguza uzito kutokana na mazoezi makali aliyofanya kujiandaa na pambano hilo linalovuta hisia za mashabiki wa ngumi duniani.

 “Jambo la msingi ambalo nitafanya siku ya Jumamosi ni kufurahia mchezo huu. Ni siku kubwa katika sehemu ya maisha yangu, najiona nimerejea na nguvu mpya,” alisema Fury muda mfupi baada ya kupima uzito.



Chanzo: mwananchi.co.tz