Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fury: Niko Tayari Kumkabili White

Skysports Tyson Fury Boxing 5441196 Tyson Fury yuko tayari Kuzichapa na Dillian Whyte

Sun, 17 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamasumbi wa uzito wa juu Tyson Fury amemsifu mpizani wake Dillian Whyte kwenye uwanja wa Wembley kwenye mpambano wao wa wikeindi ijayo na amesema yuko tayari kumkabili.

Mpiganaji huyo asiyepigika anatarajia kukabiliana na muingereza mwenzie kwenye mpambano huo, ambapo yeye anasema kuwa ni pambano lake la fainali huku akiwa na rekodi ya kupambana mapambano 31, huku akiwa hajapoteza hata pambano moja na akitoa sare pambano moja tu.

“Whyte ni mpiganaji mzuri, ni mtu asiyezuilika kwa muda mrefu, ni mtu ambaye wapambanaji wengi wanamkimbia. Hakuna anayetaka kupigana na Dillian Whyte kwa sababu yoyote, anapiga ngumi mbaya sana, anapiga ngumi sehemu muhimu, ni mtu mgumu na imara.

Anarekodi nzuri ya kupoteza mapambano mawili. Tiketi zate zimeuzwa saa chache kabla ya pambano, kwa hiyo ni mpambano wa kuvutia, na siwezi kusubiri kutoa burudani nzuri.” Alisema Tyson Fury

Mpambano kati ya Tyson Fury na Dillian Whyte unakwenda kuweka rekodi ya uwanja wa wembley ya kupata watazamaji wengi zaidi ambapo haijawi kutokea kwenye uwanja huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live