Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Francis Ngannou: Kutoka sifuri mpaka Tsh bil 25 kwa siku

Francis Ngannou Ggv Francis Ngannou.

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiacha stori juu ya kupoteza pambano lake dhidi ya Tyson Fury Juma lililopita , nyuma ya pazia yapo mengi ya kujifunza na kuongezea kwenye huo unaoitwa mchakato kama ambavyo ProjectTheFuture imekuwa ikiamini.

Francis Ngannou anajadiliwa sana juu ya kupokwa ushindi lakini kitendo cha yeye kupanda tu ulingoni kabla hata ya pambano kuanza ukilink na stori ya alipotoka ulikuwa ni ushindi tosha kwake.

Kwao Cameroon Ngannou alikuwa miongoni mwa vijana waliotoka kwenye maisha duni kama ni bongo ni sawa na kusema chini ya dola moja.

Harakati zake za utafutaji kwenye machimbo alichagua kuzifanya daraja na kusave kila anachopata akiamini ipo siku atakuwa bingwa wa masumbwi kama alivyo Mike Tyson bondia anayemuhusudu Ulimwenguni.

Katika umri wa ujana alijaribu mara kadhaa kuzamia Ulaya kupitia boda la Morocco bila mafanikio kila wakati alinaswa na watu wa usalama.

Baada ya majaribio mengi alifanikiwa kuingia Hispania lakini mipango yake ilikuwa ni kwenda Ujerumani ambapo aliamini huko atapata mafunzo ya ubondia.

Mipango haikuwa matumizi akajikuta anaishia kufanya kazi kwenye maeneo ya Gym moja huko Ufaransa.

Hakuna alichopoteza alikutana na mmoja kati ya waongoza mazoezi wa Gym hiyo akashauriwa ajifue kwenye Martial Art na huo ndio ukawa mwanzo wa Ngannou kujipata kwenye mchezo wa mapigano.

Mwaka 2021 Francis alipata moja ya mapambano makubwa alipopigana na Stipe Miovic na kufanikiwa kumpiga na kuwa bingwa wa uzito wa juu hii ni baada ya miaka 10.

Mbali na kufanikiwa kwenye Martial Art hakukata tamaa kuhusu Boxing akaanza kutafuta msaada wa Mike Tyson na alianza kupewa mafunzo ya Boxing.

Baada ya kuiva alifanikiwa kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza na kupambana na bingwa wa uzito wa juu wa Masumbwi Tyson Fury.

Majaji hawakuwa upande wa Ngannou lakini mbali na yote Ngannou amefanikiwa kuifikia ndoto yake ya muda mrefu kutoka dola moja mpaka Bilioni 25 kwa usiku mmoja kwenye Boxing! Ndoto yake ilikuwa ni kuwa Bondia (Boxer), baada ya miaka kupita amekuwa bondia.

Chagua kuamini mchakato ,kama sio pesa basi huo muda ndio mtaji wa mapambano yako kama Ngannou.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live