Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu sababu za Mwakinyo kufungiwa kupigana Uingereza

Mwakinyo Gloves .jpeg Mwakinyo

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia namba moja nchini, HASSAN MWAKINYO, amefungiwa kupigana, na bodi ya usimamizi wa ngumi nchini Uingereza (BBBC), kwa muda usiojulikana, ikiwa ni siku chache tangu apoteze dhidi ya LIAM SMITH wa Uingereza.

Kwanini amefungiwa?

Kwa mujibu wa katibu wa kamisheni ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini (TPBRC), YAHYA POLI, amesema bondia atakuwa 'Suspended' kwa moja ya sababu zifuatazo.

(1). Kwa sababu za kiafya, baada ya chama cha ngumi cha nchi husika kumpima na kugundua ana shida ya kiafya.

(2). Kupoteza pambano kwa Knock Out au Technical Knock Out.

(3). Kupoteza pambano katika namna isiyo ya kawaida, n.k.

Kufungiwa katika nchi moja kunaweza kumsababisha bondia asicheze acheze kwenye mataifa mengine, kivipi.

Iwapo chama cha nchi inayoandaa pambano kitauliza sababu ya kusimamishwa kwa bondia kwa chama kilichomsimamisha.

Iwapo sababu ya kusimamishwa kwake ikawa ni ya jumla inaweza kumfanya bondia asicheze kwenye nchi nyingine, na kinyume chake.

Bado haijafahamika ipi sababu rasmi ya kusimamishwa kwa MWAKINY0, lakini kwa sababu tajwa hapo juu uwenda ni kwa sababu alipoteza pambano lake kwa TKO au kutokana na jinsi alivyopoteza pambano hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live