Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fadhil Majiha achimba mkwara Tanzania

Fadhil Majiha Fadhil Majiha.

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia namba moja nchini Tanzania, Fadhili Majiha “Kiepe Nyani” amefunguka hakuna Bondia yeyote nchini anayeweza kupanda naye ulingoni na anayetaka kufanya hivyo anamkaribisha kwenye Gym yake ya Uwanja wa Kivita kupigana naye na siyo kama wanavyotaka wao.

Majiha ametoa onyo hilo ikiwa ni siku chache tangu ashinde mkanda wa ubingwa wa WBC Afrika, ambapo amewetaka wanaomtamani kufika kwenye gym, kwani atawapa sparing ngumu

Majiha amesema kuwa haoni sababu ya kuhangaika na mabondia wa ndani kwa kuwa siyo sehemu ya uwezo wake na kama wapo watakaomuhitaji basi wanakaribishwa katika Gym na kuwapa mazoezi makali na siyo mechi kama wanavyotaka wao.

“Hakuna ambacho wanaweza kufanya zaidi ya kuwapa mazoezi kwa sababu siyo levo yangu wakitaka hivyo waje kwenye Uwanja wa Kivita pale, tutafunga ulingo na kamera za waandishi zitakuwepo kuripoti na siyo wao hata ambao wanaona wana mapambano magumu basi nitakuwa tayari kufanya hivyo,” amesema Majiha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live