Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ezra Paulo kuleta Medali ya Shaba nchini

Fs Bondia Ezra Paulo Mwanjwango

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Ezra Paulo Mwanjwango sasa ni rasmi atapata medali ya Shaba baada ya kupoteza mchezo wake wa hatua ya nusu fainali katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana.

Ezra alipoteza dhidi ya Andrew Chilata wa Zambia kwa points za matokeo ya kurejewa 5-2 (Bout review) baada ya matokeo ya awali 3-2 katika uzani huo wa Lightweight 60kg.

Sasa wamebakia mabondia wawili wa Tanzania kucheza hatua za nusu fainali ambao ni Nahodha wa Timu Yusuf Changalawe vs Pita Kabejii wa DR Congo na Musa Wambura vs Kanouni O. kutoka Algeria ambao wate watacheza usiku wa leo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live