Ndani ya siku 8 Bondia Mandonga alipigana mapambano mawili na yote akapokea kichapo ndani ya nchi mbili tofauti.
Mandonga alianza kupigana nchini Kenya dhidi ya Wanyonyi akapigwa kwa pointi kisha Julai 29 Jijini Mwanza alikuwa na pambano dhidi ya Mganda Moses Golola kwa TKO raundi ya tatu.
Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Edo amempa ushauri huu bondia Karim Mandonga;
Kaka achana na ngumi....Wabongo wanafiki sana..wanataka ufe ulingoni waanze kuposti 'Rest in peace bro'......Kwanza akili zao zipo katika Amapiano sasa hivi.
Je wewe msomaji una neno gani kwa Bondia Karim Mandonga?mpe neno moja tafadhali