Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dullah mbabe akubali kichapo

Abdallah Pazi, Dulla Bondia Dullah Mbabe akiwa ulingoni

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Abdallah Pazi maarufu ka "Dullah mbabe" amepoteza Pambano lake kwa pointi dhidi ya Bondia kutoka nchini DR Congo, Tshimanga Katompa.

Pambano hilo la uzito wa Super Middle, limepigwa katika uwanja wa PTA, Jijini Dar es Salaa, na lilikuwa ni pambano la raundi 10.

Kabla ya Tshimanga Katompa, Dullah alikuwa apigane na Mkongo mwingine Alex Kabangu lakini pambano liliota mbawa siku chache baada ya taarifa kudai Kabangu amepata majeraha na ndipo alipotafutwa Kitompa.

Katompa amemuangusha Dullah mara tatu katika pambano hilo na ametawala takribani raundi zote 10.

Dullah amepoteza pambo lake la poli mfululizo baada ya miezi michache iliyopita kupoteza kwa bondia Twaha Kiduku.

Mwisho wa mchezo Majaji wote watatu wamlimpa Katompa ushindi wa alama dhidi ya Dullah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live