Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dullah Mbabe kuvaana na Katompa

Dullah Mbabe Mtaani Dullah Mbabe kuvaana na Katompa

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, ampa salama za ukaribisho mpinzani wake bondia Eric Katompa kutoka Kongo kuelekea pambano la marudiano "Pay back Night " linalotarajiwa kufanyika Julai 15,2023 Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Michuziblog Leo Juni 01,2023 Jijini Dar es salaam Dullah amesema pambano la awali Lililofanyika 2021 mpinzani wake Alimbahatisha hivyo watanzania wategemee kumuona akiwa kwenye ubora wake Akimchapa Mpinzani wake makonde siku hiyo .

"Kwanza namkaribisha sana Katompa yeye si mkongoman basi aje na hii itakuwa safari yake kwa mara ya 4 na hurudi tena kwa kipigo nitakachokupa na ukianika tuna aunua yani mguu wa shingo mguu wa roho tukutane Dar."

Pambano hilo la uzito wa juu la raundi 10 ambapo itakuwa kwa mara ya pili mahasimu hao wawili kupigana katika ardhi ya Tanzania ambapo pambano lake la lilifanyika mwaka 2021 jijini Dar es Salaam, Dullah Mbabe alipoteza kwa pointi.

Pia Dullah ameeleza kuwa kwa sasa yupo kambini akijiandaa kuhakikisha anafanya vizuri na kuwapa furaha Watanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live