Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dullah Mbabe amfunika Twaha Kiduku

Mbabe Pic Data Bondia Dullah Mbabe

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wwakati Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ akimfunika Twaha ‘Kiduku’ Kassim kwa ubora wa mabondia wa muda wote nchini, Hassan Mwakinyo amebakiza vihunzi viwili nchini ili kukaa kileleni.

Mwakinyo amekwaa kisiki kwa wakongwe, Rashid Matumla ‘Snake man’ ambaye mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia ‘Boxrec’ unamtaja kuwa namba moja kwenye ubora wa muda wote na Rogers Mtagwa anayekamata nafasi ya pili.

Kwa mujibu wa Boxrec, Hassan Mwakinyo ni namba tatu kwenye ubora huo akiwa na pointi 14.59 nyuma ya Matumla ambaye hadi anastaafu alikuwa na pointi 19.14 na Mtagwa pointi 17.56. Katika viwango hivyo, mabondia wawili pekee wanaocheza hadi sasa ndiyo wameingia kwenye 10 bora, mwingine ni Ibrahim Class aliyetajwa wa tisa.

Wengine ni Joseph Marwa, Francis Cheka, Francis Miyeyusho, Mbwana Matumla, Mambea Bakari na Anthony Mathias aliyehitimisha 10 bora ya muda wote nchini. Boxrec imemtaja Mbabe kwenye nafasi ya 19 akiwa na pointi 3.244.

Kiduku ameshindwa kufurukuta kwenye orodha ya mabondia bora wa muda wote akizidiwa pointi moja na Mbabe - bondia aliyewahi kumchapa mara mbili mfululizo na mpinzani wake kwenye uzani wa super middle.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz