Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dullah Mbabe, Twaha Kiduku kumtangulia Mwakinyo

Mwakinyo Gloves .jpeg Bondia Hassan Mwakinyo

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kama sio Twaha ‘Kiduku’ Kassim basi ni Abdallah ‘Mbabe’ Pazi atapindua meza kwa kumtangulia Hassan Mwakinyo kuandika historia ya kuwa bondia wa kwanza kucheza visiwani Zanzibar, tangu ngumi ziruhusiwe visiwani humo.

Unakumbuka, Mwakinyo alitangazwa kucheza pambano kuu na bondia kutoka Marekani, ambalo lingekuwa la kwanza la ndondi kupigwa visiwani humo tangu waliporuhusu ngumi zichezwe.

Pambano hilo limesogezwa mbele mara mbili, ingawa zote halikufanyika huku promota Shomari Kimbau akieleza kwamba litachezwa Aprili 28 mwaka huu.

“Kila kitu nimekamilisha na vibali vyote nilipata, ila kuna vitu vilinizuia kuendelea na maandalizi nitaviweka wazi hivi karibuni,” alisema Kimbau ambaye anashirikiana na Bakari Songoro kuliandaa.

Songoro alisema pambano hilo walishirikiana ingawa baada ya kushindikana aliomba acheze Mbabe, Machi 19 mwaka huu.

“Nasubiri majibu na Dullah atacheza na bondia wa Thailand au Italia kwenye uwanja uleule wa Mao Tse Tung,” alisema.

Inaelezwa Kiduku naye anapigiwa hesabu ya kwenda kuzichapa visiwani humo hivi karibuni lakini kupitia kwa promota mwingine.

Chanzo: Mwanaspoti